• Wasiliana Nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Baruapepe za watumishi |
    • Malalamiko |
MLIMBA DISTRICT COUNCIL
MLIMBA DISTRICT COUNCIL

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa HALMASHAURI YA WILAYA YA MLIMBA

  • Mwanzo
  • kuhusu sisi
    • Historia
      • Chimbuko/ Asili
      • Ukubwa wa eneo
      • Watu wa eneo husika
      • Hali ya hewa
      • Shughuli za kiuchumi
      • Orodha ya viongozi
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa taasisi
      • Muonekano wa muundo
    • Idara/ Vitengo
      • TEHAMA
      • Mkaguzi wa Ndani
      • Ujenzi
      • Fedha na Biashara
      • Rasilimaliwatu na Utawala
      • Kilimo na Ushirika
      • Mipango, Takwimu na ushirika
      • Mazingira na Usafi
      • Elimu Msingi
      • Elimu Sekondari
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Maji
      • Ardhi, Maliasili na Mazingira
      • Ufugaji na uvuvi
      • CHF iliyoboreshwa
      • Sheria
  • Fursa za uwekezaji
    • Vivutio vya kitalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
      • Msingi
      • Sekondari
    • Maji
    • Kilimo
    • Mifugo
    • Uvuvi
    • Huduma za watumishi
    • Rasilimali watu
    • TEHAMA
  • Madiwani
    • Orodha ya waheshimiwa madiwani
    • Kamati za kudumu za Halmashauri
      • Fedha, utawala na mipango
      • Elimu, Afya na maji
      • Uchumi, Ujenzi na mazingira
      • Ukimwi
      • Maadili
    • Ratiba
      • Vikao vya waheshimiwa madiwani
      • Kumuona mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Itakayotekelezwa
    • Inayoendelea
    • Iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria ndogo
    • Mkataba wa huduma kwa mteja
    • Mpango mkakati
    • Ripoti mbalimbali
    • Fomu mbalimbali
    • Miongozo mbalimbali
  • kituo cha habari
    • Taarifa kwa umma
    • Video za shughuli za ofisi au kitaifa
    • Hotuba za viongozi mbalimbali
    • Maktaba ya picha

maafisa kilimo wekeni malengo

Posted on: November 27th, 2020

Pichani juu: Mhandisi Emanuel Kalobelo (mwenye suti Nyeusi) akizungumza na Dr. Annete Kitambi Afisa Mifugo na Uvuvi katika banda la Halmashauri ya wilaya ya Mlimba.

MAAFISA kilimo katika wilaya zote mkoani Morogoro wametakiwa kujiwekea malengo katika uzalishaji wa mazao ya chakula na biashara ili kuufanya mkoa huo kuwa kinara ya uzalishaji wa mazao hayo nchini.

Kauli hiyo imetolewa na Katibu tawala wa mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo wakati wa uzinduzi wa msimu wa kilimo kimkoa uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika kijiji cha Njage halmashauri ya wilaya ya Mlimba.

Akimwakilisha mkuu wa mkoa huo,Mhandisi Kalobelo amesema kwa kujiwekea malengo mkoa utajua wapi kuna tatizo na litatatuliwa vipi ili kuweza kumkomboa mkulima katika mazao anayolima  na bila kufanya hivyo tutakuwa tunarudi nyuma kwani hatutakuwa na takwimu za kutosha.

Amesema kwa msimu huu wa kilimo ni muhimu kwa maafisa hao kilimo kuwakumbushia wananchi mazao gani yanafaa kwa kilimo na kwa wakati gani kwa kufanya tafiti mbalimbali za mbegu na mbolea na kwa kufanya hivyo watakuwa wamemwinua kiuchumi mkulima.

Amebainisha kuwa serikali ya mkoa huo ina mpango wa kuwakaribisha wataalamu wa utafiti wa udongo ili kubaini udongo wa maeneo mbalimbali yanafaa kwa kilimo cha aina gani lengo ni kujitathmini na kupiga hatua ya maendeleo katika maeneo yote mkoani humo.

Katibu tawala huyo pia amezikumbushia serikali za kata na vijiji kuhakikisha wanashirikiana na wataalamu wa kilimo kwa kupanga maeneo ya wakulima na wafugaji na hawatotaka kusikia migogoro ya wakulima na wafugaji.

Aidha katibu tawala huyo amezitaka halmashauri kuimarisha vyama vya ushirika ili iwe chachu katika maendeleo ya kilimo na pia wahakikishe pembejeo zote zinazohitajika zinakuwepo maeneo ya wakulima kabla ya uzalishaji.

Hata hivyo Mhandisi Kalobelo amewaomba wawekezaji kuwekeza mkoani humo ili kuweza kuchakata mazao mbalimbali na kumpatia faida mkulima wa mazao yake na kutaka maghala yote yaliyojengwa tokana na miradi mbalimbali yatumike na wawekezaji waanze kuweka mazao na sio kukaa bila mazao.

Kwa upande wao wakuu wa wilaya na wakurugenzi wa halmashauri zote mkoani humo wamemuahidi katibu tawala huyo kuhakikisha kuwa wanasimamia maelekezo ya serikali ili wakulima wake kupata mazao mengi na kufanya mkoa huo kuwa ghala la chakula.

Matangazo

  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOFAULU NA KUCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 18, 2020
  • ORODHA YA WANAFUNZI WALIOFAULU MTIHANI WA KUMALIZA ELIMU YA MSINGI 2019 HALMASHAURI YA WILAYA YA KILOMBERO December 09, 2019
  • FOMU ZA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA 2021 December 15, 2020
  • FURSA KATIKA SEKTA YA KILIMO March 27, 2017
  • Angalia zote

Habari Mpya

  • Halmashauri ya wilaya ya Mlimba yakadiria bajeti yake

    January 25, 2021
  • Madiwani sikilizeni wananchi: DC Mlawa

    December 19, 2020
  • maafisa kilimo wekeni malengo

    November 27, 2020
  • Mhandisi Kalobelo azindua msimu mpya wa kilimo 2020/2021 Wilayani Mlimba ,azitaka Halmashauri kuimarisha vyama vya ushirika.

    November 27, 2020
  • Angalia zote

Video

MAKAO MAKUU KILOMBERODC KUHAMIA MNGETA
video zaidi

Viunganishi vya haraka

  • Fomu ya maombi ya ruhusa
  • Fomu ya utambulisho benki
  • Fomu ya Kuhuisha Uanachama CHF iliyoboreshwa
  • Wasifu wa Wilaya
  • Muundo wa Halmashauri
  • Eneo la Kijiografia
  • Fursa za Uwekezaji Kilombero

Viunganishi linganifu

  • TAMISEMI
  • Utumishi
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ikulu
  • Idara kuu ya Takwimu (NBS)
  • Tovuti kuu ya Takwimu huria

kitafutio cha watembeleaji wa duniani

world map hits counter

Visitors Counter

free HitCounter

Ramani ya eneo

Wasiliana Nasi

    Mngeta Kijiji cha Itongoa

    Anuani: P.O.BOX 263

    Simu: 023 293 1523

    Mobile: 0232931523

    Barua pepe: ded@kilomberodc.go.tz

Mawasiliano mengine

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki @2017 Halmashauri ya Wilaya ya Kilombero.Haki zote zimehifadhiwa